Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri

About the product
Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hiki kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo, mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.

Mtunzi wa Kitabu hiki Charles P. M. Nazi ni mshauri wa masuala ya biashara.

Kitabu hiki ni matokeo ya utafiti na uzoefu katika kazi za ukaguzi alizozifanya kwa kuangalia matatizo ya uendeshaji wa biashara mbali mbali pamoja na ushauri alioutoa kwa watu waloomba ushauri kutoka kwake.

Price
6,000
Contact with supplier
BACK TO TOP